Ukimuona kwa jinsi alivyo mrembo na sura ya kike kweli, huwezi kudhania kuwa, Hannah Winterbourne alizaliwa mwanaume.
Ni mwanajeshi mahiri aliyefanya kazi kwenye maeneo ya vita nchini Afghanistan na sasa ameamua kujitokeza kama mwanajeshi wa kwanza nchini Uingereza kuwahi kubadilisha jinsia yake.
Hannah enzi akiwa mwanaume
Ni ofisa wa jeshi kitengo cha Royal Electrical and Mechanical Engineers nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 27 aliyetumikia jeshi katika miaka yake ya kwanza kama mwanaume kabla ya kuamua kubadilisha jinsia na kuwa mwanamke.
Anadai alipokuwa mtoto alijihisi kuwa mwili wake haukuwa sawa kama watoto wengine wa kiume na umri ulivyoenda ndipo alipozidi kugundua kuwa huenda akawa mwanamke.
Baada ya kumaliza mafunzo ya jeshi na kisha kupelekwa Ujerumani ndipo alipowaambia madaktari kuanza kubadilisha jinsia. Baada ya kuhamishiwa Catterick Garrison, North Yorkshire, ndipo alipoanza kuishi wazi kama mwanamke baada ya kufanyiwa hormone therapy, kufanyiwa upasuaji na ndevu zake kuondolewa.
“Kwa kupitia hormone therapy na upasuaji kadhaa, wameniruhusu kuubadilisha mwili wangu kiasi kwamba najisikia furaha kutembea mtaani kama mwanamke,” aliliambia The Sun.
“Watu wanaona mwanamke na wanazungumza na mimi kama mwanamke. Inanifanya nijiamini mwenyewe.”