MWANADADA asiyeishiwa habari, Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anadaiwa kujutia mimba yake aliyopachikwa na aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ wakati wa mapenzi yao.
Chanzo makini kilicho karibu na Wema kilieleza kwamba, mwanadada huyo kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu huku akijutia mimba aliyopewa na Kanumba ambayo ilichoropoka kwa bahati mbaya na huyo ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito.
“Hii yote inatokana na kwamba kwa sasa anatamani kuitwa mama lakini hapati hivyo kujikuta akiukumbuka ule ujauzito wa Kanumba anateseka kweli moyoni,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Wema kuhusu ishu hiyo alikiri na kuonesha namna gani anateseka moyoni.
“Nateseka kweli, tangu ilipotokea kwa Kanumba haijawahi kutokea tena. Hakuna mtu ambaye hapendi kuwa mama, nazidi kumuomba Mungu huenda na mimi itatokea nitapata,” alisema Wema