Wakizungumza na Waandishi wa habari muda mchache baada ya kutulizwa kwa vurugu hizo na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Geita Bw.Joseph Msukuma kasheku aliyefika kwenye eneo la tukio na kusuruhisha mgogoro huo ambapo baadhi ya wachimbaji madini wamelilalamikia jeshi la polisi kwa kushindwa kufuata misingi ya uwajibikaji kwa kupora mali za wananchi na kuwafukuza kwenye maeneo yao waliokodishwa kwa gharama ya shilingi 200,000 baada ya kubainika madini ya dhahabu yapo kwa wingi kwenye maeneo hayo.
Akizungumza baada ya kusuruhisha mgogoro huo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Geita Bw.Joseph Msukuma Kasheku amesema kuwa mgodi huo umefungwa kwa muda ili wachimbaji wadogowadogo wapate mikataba ya kuendelea na uchimbaji kutokana na fedha walizolipia huku akiwataka wachimbaji wa kati waondoe magari yao kwenye maeneo hayo ili haki itendeke.
Akijibu tuhuma zinazowakabili baadhi ya askari polisi mkoani Geita wanaotuhumiwa kupora madini ya dhahabu kilo kumi na tano kamanda wa polisi mkoa wa Geita Bw.Joseph Konyo amezungumza na Mwanahabari wetu kwa njia ya simu akidai kuwa askari wameenda eneo la machimbo kusimamia amani na kwamba madini ya Dhahabu yana yogombaniwa yamekabidhiwa kwa afisa madini wa mkoa ili aweze kuthaminisha kwa ajili ya kutozwa kodi ya serikali kisheria.