Tuesday, January 20, 2015

WANAFUNZI WAPIGWA MABOMU YA MACHOZI WAKITADAI KIWANJA CHAO CHA KUCHEZEA

Polisi nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya kutoa machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na mmiliki binafsi.

Polisi hao wakiwana Mbwa waliwatawanyta wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuuangusha ukuta mpya uliojengwa kati ya shule yao na uwanja huo.
Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa uzio.
Shule hio ina karibu watoto 1,000 walo kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji.

Baraza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa ujenzi
AUNT EZEKIEL ACHUKIZWA NA MABISHANO YA KIDINI YALIYOZUKA BAADA YA POSTI YAKE!