MIMI ni Mmatengo, kabila moja kubwa katika mkoa wa Ruvuma, lakini lisilo maarufu, tunapatikana katika wilaya kubwa pia, inaitwa Mbinga. Idadi kubwa ya wamatengo ni wakristo, tena wa madhehebu ya Roman Catholic.
Katika moja ya vitu ambavyo wanakijiji wenzangu wanaviheshimu sana, ni makaburi. Wenyewe wanaita Shamba la Bwana. Ili kuonyesha heshima hiyo, makaburi yamepewa ‘ofa’ ya kujengwa mbali kabisa na makazi ya watu, tena miti mikubwa na ile ya maua imepandwa kuyazunguka.

Katika kipindi kigumu ambacho mtu anakabiliana nacho katika maisha yake, makaburi ni kimbilio lake. Pombe hupikwa, mbuzi huchinjwa na watu wa ukoo pamoja na ndugu wengine, hutembelea makaburi na kuyafagia.
Baadaye sala maalum ya maombi hufanywa ya kuomba kuondolewa kwa mikosi, balaa na vitu vingine, kitu kinachoaminika kufanywa na mizimu ya marehemu wapendwa wetu waliozikwa hapo!
Baadaye sala maalum ya maombi hufanywa ya kuomba kuondolewa kwa mikosi, balaa na vitu vingine, kitu kinachoaminika kufanywa na mizimu ya marehemu wapendwa wetu waliozikwa hapo!
Utotoni, tulipewa simulizi nyingi sana zenye kututia hofu ya kuogopa na kuheshimu makaburi. Ninakumbuka simulizi moja, watoto tuliambiwa kuwa ni marufuku kuonyesha kaburi la mtu kwa kidole, eti ukifanya hivyo kidole kitakatika!
Tuliambiwa Shamba la Bwana wanaishi watakatifu na malaika wao. Makaburini ni sehemu isiyotaka kelele, yahitajika nidhamu ya hali ya juu na kamwe hapatarajiwi kuwa zogo la aina yoyote linaweza kutokea. Mambo yanafanyika kimyakimya na watu wanaondoka kimyakimya!

Na kwa kweli, sikuwahi kuonyesha kaburi la mtu yeyote kwa kidole hadi leo hii, ingawa kimjinimjini nashangaa kuona watu wanakalia makaburi ya wenzao wakati wa mazishi ya mtu mwingine!
Maisha yanabadilika sana, hasa katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia ambapo dunia imegeuka kuwa kijiji kinachotosha kiganjani.
Maisha yanabadilika sana, hasa katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia ambapo dunia imegeuka kuwa kijiji kinachotosha kiganjani.
Nawazungumzia wadogo zangu, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel ambao wiki iliyopita, wakitokea Dodoma kurejea Dar kwenye ‘mishemishe’ zao, walisimama mjini Morogoro kwa ajili ya kwenda kuomba dua katika kaburi la nyota wa Bongo Fleva, Albert Mangweha ‘Ngwea’ aliyetangulia mbele ya haki.
Alikuwa staa mwenzao, wakikutana sana kwenye kumbi za starehe na kwa maana hiyo, lilikuwa jambo jema kumuombea dua, ikiwa ni pamoja na kumuomba pia kuwatayarishia ‘kasehemu’ ili wakati wao ukifika (kila nafsi itaonja mauti) wasipate taabu!

Wakiwa na wapambe wao (wote wanaume) akina dada hao walikaa wakipeana ubavu, wakiliweka kaburi ya mkali huyo wa freestyle katikati, kisha wakaanza kupiga stori zilizoambatana na vicheko, wakati mwingine vya kuvunja mbavu kabisa.
Huenda ni ukisasa au labda kuondoka kwa hofu ya kifo. Lakini katika hali ya kawaida, siyo jambo la kutegemea kumuona mtu, tena msichana kama walivyo hawa wadada, halafu Wabantu, wakipiga soga, wakituma sms kwa simu zao na kuangua vicheko juu ya kaburi!

Ni kweli, hatuwezi kukwepa kwenda na wakati, lakini siyo kila jambo kwetu kama Waafrika, ni wakati muafaka. Wazungu, kwa utamaduni wao, siyo jambo la ajabu kwa mzazi kuogelea na bintiye aliyevunja ungo, lakini ni ujuha, kuuleta utamaduni huu kwetu, kwa sababu ni kitendo cha aibu na kisichokubalika.
Pengine ni utoto, maana baadhi ya mambo yanayofanywa na hawa wadada, yanashangaza kidogo na inawezekana pia, ni kukulia sana maisha ya mjini. Kama Brad Pit anakula denda na Angeline Jolie makaburini katika filamu, hakuna ubaya, katika maisha halisi, Wabongo kuangusha vicheko vya kufa mtu makaburini?
Lazima tuseme hapana, vipo vya kuiga, vipo vya kukataa. Utandawazi hauwezi kutuondolea asili yetu, mwanamke lazima aendelee kuonyesha ishara ya kupiga magoti ya heshima anapomsalimia mwanaume mtu mzima, kwa sababu ndiyo mfumo wetu na wala hii siyo dharau dhidi yao.
Kama leo Wema na Aunt wanaangua soga juu ya kaburi la mpendwa wao, pata picha watoto wao watakuwa na tabia gani makaburini! Hata hivyo, huwa najiuliza, vituko kama hivi ni ili iweje sasa?