Mpaka Jumatano usiku watu waliokua wamefariki kwenye ajali hii ni 31 huku 12 wakiwa hawajulikani walipo baada Ndege inayoimilikiwa na Shirika la Taiwan la TransAsia kupata ajali na kuangukia kwenye mto katika mji wa Taipei.
Taarifa zinasema kuwa watu 58 walikuwa ndani ya ndege hiyo, huku watu 16 wameokolewa na kupelekwa Hospitali na wengine 10 bado wamenasa katika ndege hiyo ambapo waokoaji wamelazimika kuikata ndege hiyo ili kuwaokoa watu ambao bado wapo ndani.
Picha zinaonyesha ndege hiyo ikiwa imezama kwa kiasi kikubwa katika mto Keelung, ndege hiyo ilipita karibu na magari na kudondoka mtoni muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Songdshan, Taipei kuelekea uwanja wa ndege wa Kinmen nje ya Taiwan huku chanzo cha ajali kikiwa bado hakijajulikana.