ALIYEKUWA meneja wa baa ya Vijana Social ya mjini Morogoro iliyokuwa ikimilikiwa na Bondia Francis Cheka, Bahati Kabanda aliyemponza hadi kuhukumiwa kifungo, hivi sasa anaishi kwa hofu kutoka kwa mashabiki wa bingwa huyo wa masumbwi wa dunia.
Cheka alikutwa na hatia ya kumpiga ngumi na kumuumiza meneja wake huyo, wakati alipokwenda kwa ajili ya kufuata fedha za mauzo ya baa yake hiyo lakini wakapishana maneno yaliyosababisha tukio hilo lililowashtua watu wengi.
Bondia Francis Cheka (kulia) akiwa amepanda ndani ya gari la polisi baada ya kuhukumiwa miaka mitatu jela kwa kumpiga meneja wa baa yake ambapo atamlipa fidia ya sh. milioni moja. Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Morogoro.
Licha ya mashabiki wa bondia huyo aliyemaliza enzi za Snake Boy, Rashid Matumla, watu wengine wanaodaiwa kumpa hofu Baraka ni pamoja na wakusanya chupa za plastiki ambao walimtegemea Cheka kwa ajili ya kwenda kuziuza katika kiwanda chake kilichopo maeneo ya Kihonda mjini hapa.
...Akipanda gari kwenda jela.
“Ukweli maisha ya huyu jamaa hapa Morogoro ni magumu sana kwa sababu kila anakokwenda anakutana na watu wanaomnanga juu ya kitendo alichokifanya. Watu wanaomtakia mema wanamshauri kuwa mwangalifu sana wa nyendo zake kwani watu wanaweza kumfanya lolote maana Cheka ni mtu muhimu sana hapa,” alisema shuhuda mmoja.