Saturday, February 7, 2015

AUNTY LULU AWAENDEA KWA BABU WABAYA WAKE

MWIGIZAJI asiyekaukiwa matukio Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa amekwenda kwa mganga (babu) Mtwara kwa ajili ya kuweka zindiko wabaya wake wasimsumbue.
Staa wa Filamu za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’.
Akipiga stori na mwanahabari wetu, Aunty Lulu alisema kuna wabaya wake wamekuwa wakimfanyia ‘mambo’ mabwana zake wayeyuke hivyo hayupo tayari kuona nyota yake inafifia.
“Nimeona bora nikarekebishe kidogo maana mjini kila kukicha watu wanakutafuta na kukuharibia mambo yako, niko fiti sasa,” alisema Aunty Lulu.