Monday, February 2, 2015

HABARI KAMILI:BONDIA CHEKA ATUPWA JELA MIAKA MITATU

Bondia Francis Cheka (kulia) akiwa amepanda ndani ya gari la polisi baada ya kuhukumiwa miaka mitatu jela kwa kumpiga meneja wa baa yake ambapo atamlipa fidia ya sh. milioni moja. Hukumu hiyo ilitolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Morogoro.
Cheka akiongea jambo wakati akipanda gari la polisi.
...Akipanda gari kwenda jela.
Polisi (kushoto) akimwamuru Cheka kutoongea na simu.
Mdogo wake Cosmas Cheka (kushoto) akilia.
...Akiichukua simu ya cheka kutoka mfukoni.
Cheka akikabidhiwa ufunguo wa gari na Meya wa Ilala, Jerry Silaa baada ya pambano ambalo mshindi alipewa gari
Cheka akiwa na baadhi ya mikanda yake ya ubingwa
Bondia Francis Cheka akiongea na wanahabari baada ya kumchakaza Thomas Mashali tarehe 1 Mei, 2013 katika ukumbi wa PTA jijini Dar Es Salaam.(Picha na Maktaba)
BONDIA maarufu nchini wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela na kutakiwa kulipa fidia ya Sh. millioni 1 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake (Cheka) iitwayo Vijana Social iliyopo Morogoro Mjini.
Akimsomea mashitaka, Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Morogoro, Said Msuya alisema Cheka alikutwa na hatia ya kumpiga aliyekuwa meneja wa baa yake aitwaye Bahati Kabanda 'Masika'.
Alisema kuwa Cheka alitenda kosa hilo Julai 2, mwaka jana ambapo meneja huyo alikwenda kwenye baa hiyo kudai fedha zake alizokuwa hajalipwa na bondia huyo wakati akifanya kazi ya umeneja katika baa yake hiyo.
Hakimu Msuya alisema kuwa Cheka alikataa kumlipa na kumshushia kipigo kilichosababisha kulazwa hospitalini.
Baada ya hukumu hiyo huku Cheka akipandishwa kwenye difenda tayari kupelekwa gerezani akionekana kutokuwa na wasiwasi wowote, mashabiki wake walimvaa meneja huyo wakitaka kumshushia kipigo hivyo kuibua taharuki mahakamani hapo.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki hao walikuwa wakisema wapo tayari kujichanga ili kukata rufaa wakiamini kuwa bondia huyo ameonewa.
Mbali na hukumu hiyo mahakamani hapo, kulikuwa na kesi nyingine mbili zilizokusanya umati, moja ikiwa ni ya Sheikh Ponda juu ya uchochezi na ile ya mtoto wa boksi inayowakabili baba na mama Nasra.