Sunday, February 8, 2015

HATIMAYE WEMA AAAMUA KUOLEWA NA KUTULIA

Wema Sepetu amechoka
uhusiano wa boyfriend na girlfriend. Muigizaji
hiyo wa filamu amesema anataka kuolewa.
Wema alisema hayo jana kwenye reality show
yake, In My Shoes baada ya meneja wake Martin
Kadinda kumuuliza kwanini hana ‘kiki’ kwa sasa.
Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 alisema
kuna vitu vingi anataka kuvifanya ikiwemo kuwa
na hamu ya kutulia na kuwa mke wa mtu.
Hata hivyo Wema alisita kumweka wazi
mwanaume anayetaka kumweka ndani na
kumtaka meneja wake kuwa na subira.