Tuesday, February 10, 2015

HII HAPA REKODI MPYA YA MAN UTD BAADA YA MIAKA MINGI

daley blind
Klabu ya Manchester United imeendelea kutowaridhisha mashabiki wake baada ya mfululizo wa matokeo ambayo si mazuri ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata, mpaka sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.
Moja kati ya rekodi ambazo mashabiki wa United hawatazipenda ni ile inayoonyesha kuwa timu hii haijaweza kushinda mchezo hata mmoja ambao imeanza kuruhusu bao kufungwa na mpinzani wake.
Katika msimu huu United wameruhusu bao la kwanza la mchezo kufungwa na mpinzani katika michezo nane tofauti na hadi sasa hakuna mchezo wowote kati ya hiyo ambaoUnited imeweza kurudi na kushindwa zaidi ya kuambulia sare kama si kupoteza.
Katika ya mechi hizo United imeweza kusawazisha mara tano ambapo michezo hiyo iliisha kwa huku ikipoteza mchezo katika michezo mitatu iliyosalia.
wayne rooney
Michezo ambayo imeisha kwa sare baada ya United kufungwa bao la kwanza ni dhidi yaChelseaWest Brom, Aston VillaStoke City na West Ham United huku wakipoteza michezo dhidi ya Manchester City, Swansea na Southampton.
Katika miaka ya nyuma United ilijijengea umaarufu kama timu ambayo ilikuwa haikubali kirahisi kuondoka uwanjani bila kushinda mchezo na mara nyingi walishinda mechi ambazo awali ilionekana kama wangepoteza kabla ya kurudi mchezoni na kushinda mchezo karibu na mwisho wake.
Hii ilizoeleka kipindi wakati Sir Alex Ferguson akiwa kocha na hata alipokuja David Moyes bado United ilifanikiwa kushinda michezo minne ambayo ilianza kufungwa mapema.
giggs
Katika msimu wa mwisho wa Sir Alex Fergusson, United walionekana kuwa wataalamu wa kushinda mechi ambazo zingeweza kuwa za kupoteza baada ya kurudi mchezoni kwa kusawazisha na kufunga bao au mabao ya ushindi katika mechi zisizopoungua tisa ikiwa idadi kubwa ya matokeo ya aina hiyo katika miaka yote 26 ambayo United ilikuwa chini ya ‘babu’.