Tuesday, February 10, 2015

MBONGO AUAWA NCHINI UJERUMANI. KWA KUWEKEWA SUMU.

MTU mmoja anayeaminika kuwa ni Mtanzania,
Robert John Mpwata (34 ) anadaiwa kuuawa
kwa kuwekewa sumu na mwili wake kukutwa
chumbani kwake katika Mji wa Shorten nchini
Ujerumani siku chache zilizopita.
Habari kutoka kwa baadhi ya marafiki zake
waliopo huko, zinasema Robert aliyekuwa
mwanamichezo aliyecheza sarakasi, karate na
judo, aliwasiliana nao kwa njia ya simu mara
kwa mara na walipata taarifa za kifo chake
siku saba ya kufariki dunia.
Inadaiwa kabla ya kifo cha mwanamichezo
huyo, alikuwa akiwasiliana vizuri na wenzake,
lakini umauti wa ghafla uliomkuta na
mazingira yake, unawapa hofu kuwa huenda
alifariki baada ya kuwekewa sumu.
Inadaiwa kuwa Februari 8, mwaka huu ilikuwa
ni siku waliyotakiwa kufanya onyesho , kitu
ambacho kiiwafanya wawe na mawasiliano ya
mara kwa mara .
Mwandishi wa habari hii aliwasiliana na
ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani ,
ambako mfanyakazi mmoja aliyekataa kutajwa
jina lake kwa vile siyo msemaji , alikiri kusikia
taarifa hizo , lakini akasema inakuwa vigumu
kwao kutoa msaada kwa vile taarifa isiyo
rasmi inasema marehemu alikutwa na
vielelezo vinavyomtambulisha kuwa ni mtu wa
Somalia.
Robert John Mpwata akiwa na mke wake .
Naye Mwenyekiti wa umoja wa Watanzania
nchini humo , Mfundo Peter Mfundo alikiri
kutokea kwa kifo hicho, kwani awali
marehemu aliwaaga Watanzania wenzake kuwa
ataondoka kwenda nyumbani kwa mke wake .
“ Mimi nilipata taarifa kutoka kwa rafiki yake wa
karibu baada ya wiki mbili tangu akutwe
amefariki , hakuna anayejua kilichomuua
maana serikali bado haijatoa majibu. “ Mpaka
sasa bado tunasubiri kutatokea nini na hata
kama ikitokea tupewe maiti kuisafirisha ni kazi
kwani ni zaidi ya shilingi milioni 12,
nimewasiliana na baba yake anasema hana
nauli ya kumleta huko.
“ Robert alikuja hapa katika shughuli za sanaa
na alimuoa Mjerumani aliyezaa naye mtoto
Daniel ambaye ana umri wa miezi minne ,”
alisema kiongozi huyo. Kwa mujibu wa Peter ,
mke wa marehemu aliwaambia kwamba
angependa amzike mumewe nchini humo ili
iwe rahisi kwa mtoto wake kuhani kaburi lake.
Ndugu zake marehemu Robert John Mpwata
wakiwa Bongo, ( mwenye shati jekundu ni
baba yake) .
John Mpwata (65 ), baba mzazi wa marehemu
akiwa nyumbani kwake Manzese Kilimahewa
jijini Dar, alisema taarifa za kifo hicho
zimemuumiza. “ Mwanangu aliondoka mwaka
2007 kutafuta maisha huko Ujerumani na kwa
mara ya mwisho niliongea naye Desemba 22,
mwaka jana , aliniambia atakuja nyumbani na
mkewe Mzungu hivi karibuni baada ya
mwanaye Daniel kuanza kutembea .
“ Lakini cha kushangaza hivi karibuni nimepata
taarifa ya kifo chake, sina jinsi maana
nimeambiwa uwezekano wa mwili kuletwa ni
mdogo na ningependa kwenda kumzika lakini
sina milioni 2 . 5 za nauli , ninawaomba
Watanzania wanisaidie nikamzike mwanangu , ”
alisema na kutaja namba zake za simu kuwa
ni 0689 476408 au 0713 432088 .