Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba za Jengo la ghorofa tatu la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo Mtaa wa Moscow na Libya eneo la Posta Jijini Dar es Salaam na kuteketeza mali kadhaa.
Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi.Jeshi la Polisi liliwahi kufika eneo la tukio kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo huku magari ya zimamoto nayo yakiendelea kuwasili kupambana na moto huo..
Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto vikiwasili eneo la tukio.
Baadhi ya wasamaria wema wakiondoa gari iliokuwa jirani na jengo linaloteketea kwa moto
Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio,huku wananchi nao wakishuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Moja ya Gari la zimamoto likiwa limewasili eneo la tukio