Saturday, February 7, 2015

MONALISA: NITAOLEWA MWEZI DESEMBA

MKONGWE kwenye sanaa ya filamu Bongo, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ amesema baada ya kuchoka kuulizwa anaolewa lini, ameamua bora iwe mwezi wa 12.
Mkongwe kwenye sanaa ya filamu Bongo, Yvonne Cherry ‘Monalisa’.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Monalisa alisema kutokana na hilo, kama mambo yatakwenda sawa, mwezi wa tano taratibu zitaanza na kila mmoja atamjua mumewe mtarajiwa atakayefunga naye ndoa Desemba, mwaka huu.
“Nimechoka kuulizwa kila siku unaolewa lini, ni hivi, piga ua mwaka huu. Itabidi niongee na mwenzangu na nina hakika atanikubalia, mambo yatatimia tu,” alisema Monalisa.