Monday, February 16, 2015

MOTO WATEKETEZA VIWANDA, MADUKA ENEO LA KIBANGU JIJINI DAR

Moto ukiteketeza maduka yaliyokuwa jirani na viwanda vilivyoteketea Kibangu.

Vibanda vikiteketea kwa moto eneo hilo.

Moto ukiwa umetanda eneo hilo.

Magari ya zimamoto yakiwasili eneo la tukio japo kwa kuchelewa.

Baadhi ya bidhaa zilizookolewa kutoka eneo hilo.

MOTO mkubwa uliozuka eneo la Kibangu, Ubungo jijini Dar es Salaam umeteketeza viwanda vya kusaga plastiki, kuchomelea, useremala na kuunguza maduka mawili ya karibu pamoja na vibanda vingine vya biashara eneo hilo.
Moto huo umeteketeza vitu vingi vya thamani vikiwemo mashine za kulanda mbao, kusaga plastiki na za kuchomelea vyuma.
Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika mpaka sasa.