Monday, February 9, 2015

NI IVORY COAST 2015, TEMBO WABEBA NDOO YA AFCON

Yaya Toure (centre) celebrates having won the Africa Cup of Nations with the Ivory Coast, following a penalty shoot-out win over Ghana

TIMU ya Taifa ya Ivory Coast imetwaa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Ghana kwa penalti 9-8 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Bata, Equatorial Guinea.

Historia imejirudia, baada ya Tembo kuwaunga ten Black Stars kwa penalti katika fainali kama ilivyokuwa 1992 walipotwaa taji lao la kwanza.
Shujaa wa Ivory Coast usiku huu alikuwa ni kipa Boubacar Barry aliyefunga penalti ya mwisho, akitoka kuokoa ya kipa mwenzake, Razak Braimah na kumaliza kiu ya miaka 23 ya taifa lake kusubiri taji hilo.
Penalti za Ivory Coast zilifungwa na Aurier, Doumbia, Yaya Toure, Soomon Kalou, Kolo Toure, Kanon, Bailly Serey Die na Barry, wakati Wlifried Bony na Tallo walikosa mbili za kwanza.
Penalti za Ghana zilifungwa na Mubarak Wakaso, Joedan Ayew, Andre Ayew, Mensah, Agyemang-Badu, Afful, Baba na Boye wakati Acquah, Achwampong na Brimah walikosa.  
Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang, Rais wa FIFA, Sepp Blatter na Rais wa CAF, Issa Hayatou walikuwepo uwanani na awali walikagua vikosimkabla ya kukabidhi Medali na taji kwa washindi baada ya mechi 
Kikosi cha Ivory Coast kilikuwa; Barry, Bailly, Aurier, Kanon, Toure, Tiene/Kalou dk114, Die, Toure, Gradel/Doumbia, dk66, Bony na Gervinho/Tallo, sk120. 
Ghana; Razak, Boye, Rahman, Mensah, Afful, Mubarak, Acquah, Ayew, Atsu/Acheampong dk115, Gyan/Agyemang-Badu dk120 na Appiah/Ayew dk98.
The Ivory Coast team and staff pose with their Africa Cup of Nations trophy having defeated Ghana 9-8 on penalties on Sunday night
Wachezaji wa Ivory Coast na viongozi wao wakifurahia na Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa penalti 9-8 dhidi ya Ghana usiku huu
Manchester City striker Wilfried Bony holds up hero Boubacar Barry (centre), who scored the winning penalty in the final in Bata 
Mshambuliaji wa Manchester City, Wilfried Bony akiwa amembeba kipa Boubacar Barry baada ya kufunga penalti ya mwisho mjini Bata