Tukio ambalo lilishtua wengi mwisho wa wiki iliyopita ilikuwa ni ajali ya moto iliyotokea maeneo ya Kipunguni Dar es Salaam ambapo watu sita wa familia moja walifariki baada ya nyumba yao kuwaka moto usiku wakiwa wamelala.
Imehuzunisha wengi, leo ilikuwa siku ambayo ndugu, jamaa walikutana kufanya mazishi ya marehemu hao katika Makaburi ya Airwing, Dar es Salaam.