Hii imeshtua wengi walioisikia, kwa wale waliobahatika kuitembelea basi ni mashuhuda kwamba watu wengi wa kutoka jamii hiyo wamekatwa vidole na ndugu yoyote wa marehemu anakatwa vidole, umri sio kitu kinachoangaliwa sana hivyo hata watoto pia wanaguswa na hii moja kwa moja.
Hapa vidole vinakatwa kwa shoka, vipande vilivyokatwa vinachomwa moto halafu majivu yanahifadhiwa au kuzikwa pamoja na mwili wa marehemu.
Jitihada zimeanza kufanywa ili kuzuia utamaduni huo ambao madhara yake yameanza kuonekana kwa sasa