Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara akiwa na nahodha Yaya Toure wakati wakilitembeza kombe kwa mashabiki
Wachezaji wa Ivory Coast wakishangilia ushindi huku wakilindwa na wanajeshi
Maelfu ya mashabiki wa soka nchini Ivory Coast wamefika kuwapokea mabingwa wa mataifa ya Afika Ivory Coast baada ya kuifunga Ghana kwa njia ya penati na kunyakua kombe hilo.
Maelfu ya mashabiki walitanda mitaani ili kuwalaki wachezaji na viongozi kwa ushindi huo,Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara amewapongeza wachezaji na kusema ushindi wa Ivory Coast utaleta umoja na amani kwa nchi.
Polisi ilibidi kuamuru watu kubaki majumbani kwao sababu ya usalama baada ya uwanja uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya kuwalaki wachezaji na viongozi baada ya ushindi wa kihistoria wa kushinda kombe la mataifa ya Afrika huko Guinea ya Ikweta.