Kabla sijamwagika, ieleweke tu kuwa mimi nipo kwenye hii industry pia, na ninakaribisha walio kwenye hii game wachallenge hoja, simaanishi mashabiki au wasikilizaji wa muziki, bali producers na waimbaji.
Kwanza nitoe somo kuhusu sauti:
Kuna aina 2 za sauti kwenye uimbaji - 1) Long Wave na 2)Vibrating Wave. Waimbaji wote wenye sauti nzuri wanaangukia kwenye hizi category 2 na wale wenye sauti mbaya wanaangukia kwenye category ya kwanza (Long wave) ila wakiwa na kasoro hasa za kibailojia upande wa makoo, pua na sauti zao kwa ujumla.
Long wave: Hii ni sauti iliyonyooka bila mawimbi. Mfano wa wasanii wenye sauti ya hivi hapa bongo ni Vanessa Mdee, Lady Jay Dee, Ommy Dimpoz, Bob Junior na Ulaya ni Chris Brown, Justine Bieber, Taylor Swift n.k.
Vibrating Wave: Hii ni sauti yenye mawimbi hasa mwishoni mwa maneno/sentesi na ndio sauti tamu zaidi duniani. Kibongongo tunao Ali Kiba, Diamond, Ben Pal, Linah, Vumi na Ulaya ni kv; Rihanna, Beyonce, Adele, Bruno Mars n.k.
Sauti mbaya ya muimbaji husababishwa na vifuatavyo:
Haimbi kwa sauti inayotoka tumboni, anaimbia kwa kutumia koo la sauti ambalo matumizi yake ni sauti ya kuongea katika hali ya kawaida...na mwingine huharibu zaidi kwa kuipitishia hiyo sauti puani, na kwa ujumla wako kwenye category ya Long wave. Wengi nyimbo zao zimejaa Autotune (ubadilishaji wa uhalisia wa sauti unaofanywa na Producer) na Voice-overs nyingi (unaskia ni kama kwaya wakati anayeimba ni mmoja), yote hii ni kuficha ubaya wa sauti. So sauti zingine huenda ziliumbwa kwaajili ya fani ya kutangaza mpira au kuongoza jeshi la mgambo, sema ndio hivyo...riziki popote.
Sasa kwa hapa bongo wafuatao ndio wenye sauti mbaya:
Shetta
Aika (huyu namjua kwa ukaribu zaidi maana few months back nilikuwa "friends with benefit" na dada yake mkubwa pale Arusha)
Shilole
Mina
Snura
Joh Makini (huyu ni ngumu kufocus kwenye ubaya wa sauti yake kwasababu ana art kwenye uimbaji wake, anacheza maneno, illa ubaya wa sauti yake ni kuitolea puani. Na hili swala liko nje ya uwezo wa mtu kiujumla maana ndio maumbile ya sauti yake)
Karibuni kwa mchango/kuongezea wengine.