Thursday, February 5, 2015

WEMA SEPETU NI NANI MPAKA KUWA NA USHAWISHI NAMNA HII..... HII INASHANGAZA SANA..MSOME HAPA ZAIDI

Kwa mara ya kwanza kwama najitokeza kuuliza swali ambalo nahisi majibu ninaweza kuwanayo ila labda sijajua kuwa haya nilionayo ndio majibu sahihi..(Siunakumbuka enzi za soma hadithi hii kisha jimu maswali hapo chini....). Leo hii nataka kukuja hivi huyu Wema Sepetu ni nani? kwamaana kuwa anafanyanini hapa nchini hadi kuwa mtu maarufu kihivyooooo na hadi kuwa na mashabiki ambao wameapa kumpenda na kusapoti kila anachokifanya hata kama ni Negative (mara nyingi huwa -)......Mbali ya wale wanamfuatilia kupitia magazeti ya UDAKU (uswazi ndio wengi hawa)..kwenye mitandao ya kijamii kama FESIBUKU, TWITA na INSTAGRAMU kuna vikundi na watu mmoja mmoja wanao simama upande wawema kwamajiana tofautitofauti...Kwapamoja wanajiita TEAM WEMA (Naamini wanaisoma hii)



Huyu ndio wema ninaye mjua mimi!!
Kwakifupi mimi binafsi nilimsikia Wema Sepetu kwa mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2006 akiwa mshindi wa taji la MISS TANZANIA 2006....(Kama unakumbuka ushindi wake uliandamwa na kashfa za rushwa za ngono, na fitina kibao)..Baada ya hapo hakufanya vizuri kwenye mashindaono ya MISS WORLD ya mwaka huo akiwa kama mshiriki kutoka TANZANIA. (Enzi hizo nahisi Diamond alikuwa hana hata Simu ya mkononi)

Baada ya hapo zikafuata kashfa mbalimbali za Ku-DATE na mstaa Kadhaa kuanzia wa muziki, maigizo, Madingi nk (List ya majina ni ndefu sana itatujazia page)
Miaka ya hivi karibuni akaibukia Bongo Movie na kuwa muigizaji, na kacheza filamu kadhaa (Enzi za kila demu mzuri au miss anaingia kwenye tasnia). Enzi ya ZE GRETI KANUMBA (R I P, bro wewe ndio MUINZIGA HUKU)....Kama kawa huku nako alifanya vizuri kidogo (kibongo bongo)

FOMEKINGI LONGI STORY SHOTI

Hatimaye akatua kwenye mikono ya Diamond baada ya kuwa na mastaa kadhaa (Daah hapa kuna ka -list tena kabla ya Diamond)
Kwasasa ni C E O wa kampuni yake ya ENDLESS FAME (kua yake au sio yake hapa sio Ishu) inayojishughulisha ya maswala ya MOVIES PRODUCTION, NK..Ambayo aliifungua siku za hivi karibuni. Mwisho kabisa nimeambiwa anakipindi kwenye TV, sijajua kinaitwaje BUT nasikia anajizungumzia mwenyewe na maisha yake....akiwa na wale jamaa zake (and of coz bila kumsahau Meneja wake......hehehehe)
And business as usually, Kila siku yupo kwenye Media na skendo tofauti tofauti mara kagombana na huyu kisa BWANA, mara Ndugu wa Diamond hawamtaki...basi ilimladi watu wamsikie tu (Diamond alishaeleza mara kadhaa kuwa Wema huwa anazipeleka mwenyewe skendo kwa magazeti ya UDAKU-Nanasikia mwaka huu wamempa na TUZO).

Sasa kwanini nimeuliza:
Kwanza kabisa ni kweli Story za Wema ndio zinazoongoza kwa kusomwa na wapenda Udaku watu wa Blogu (Kama mimi), Magazeti ya Udaku, majarida na Radio,TV watakubaliana namimi kuwa story za huyu MDADA siauza sana (Kwahiyo zinapendwa)
Kwenye mitandao ya kijamii Wema Sepetu ana watuwengi zaidi wanao mfuatilia kuzidi mastaa wote wa hapa BONGO: Tuanze na FESIBUKU ana LIKES zaidi ya LAKI MOJA, TWITA na Followers zaidi ya ELFU THEMANINI, INSTAGRAM ana Followers zaidi ya LAKI NA ISHILINI...Hatari Sana...hakuna staa yoyote anamkaribia kwanye hili.









Akounti za TEAM Wema nazo zina watu wakutosha (Kazi yao kubwa ni kusifia na kusafisha hali ya hewa kama Wema amaichafua)
Kwamfano ipo hii inajiita WEMA REPLIES wapo INSTAGRAM (Hawa kutwa wao wema tu)




Sasa facts zipo hivi:Kwenye U-MISS; Hivi Wema anamfikia kweli Nancy Sumari ambaye alitwaa taji la Afrika?
Kwenye Kuigiza; Hivi Wema anauwezo gani wakumzidi Johari au Monalisa?
Kwenye TV: Hivi kipindichake kina ubunifu na mvuto gani? unawza kufananisha na kipindi kama wanawake LIVE,au Mkasi?

Nikweli kwamba Wema hana chakumfanya awe hivi alivyo....Naomba wadau mnisaidie kuniambia

HUYU WEMA NI NANI KUWA USHAWISHI KIASI HICHI?.