Tuesday, March 31, 2015

MTOTO WA AJABU AZALIWA SHINYANGA

Muonekano wa mtoto huyo.
WAKAZI wa Mkoa wa Shinyanga wamekumbwa na mshituko baada ya mama mmoja mwenyeji wa Ndembezi mkoani humo kujifungua mtoto wa ajabu, Amani limeinasa.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Machi 12, mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Kwa mujibu wa watu waliomwona mtoto huyo waliliambia Amani kwamba, alizaliwa akiwa na masikio yote kwenye shingo, kuanzia kidevuni kwenda kwenye paji la uso vitu vyote vimeangalia juu.
“Yaani ni mtoto wa ajabu sana. Masikio yapo shingoni. Mdomo, pua na macho vyote vimeangalia juu mpaka anatisha sana,” kilisema chanzo kimoja.Kwa mujibu wa chanzo hicho, madaktari wa hospitali hiyo wamekuwa wakiona akina mama wakijifungua watoto wa ajabu mara kwa mara lakini wanakiri mtoto huyu wa safari hii ni wa ajabu zaidi kuzaliwa katika hospitali hiyo.
“Huwezi kuamini ndugu mwandishi jana asubuhi (siku ya tukio) kwenye vikao vya kawaida vya kila siku hospitalini waliongelea kuzaliwa kwa mtoto huyo wa ajabu, ujue ni ishu nzito kwao,’’ kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, mtoto huyo aliishi katika uso wa dunia kwa saa chache na kuaga dunia huku baadhi ya ndugu wakimtaka mzazi huyo kumshukuru Mungu kwa kila jambo.
Ilidaiwa kuwa, baada ya mama mzazi kuambiwa hali ya mtoto huyo na kuoneshwa alibaki kumwaga machozi asijue la akufanya lakini alijipa moyo na kusema: “Kila jambo hupangwa na Mungu mwenyewe.”
Hata hivyo, baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema kuwa, inabidi kuomba mizimu mara kwa mara ili kuepukana na mikosi kama hiyo.