Saturday, April 4, 2015

ANGALIA PICHA_ WACHEZAJI WA SIMBA SC WATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU KITUO CHA BUHANGIJA MJINI SHINYANGA..HUU NI MFANO WA KUIGA KWA TIMU NYINGINE


Timu ya Simba Sc leo jioni imeweka historia mjini Shinyanga baada ya kuwatembelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino),wasiosikia na wasioona katika kituo cha Buhangija Jumuishi chenye watoto zaidi ya 370.Pichani ni
Msemaji wa Simba SC, Hajji Manara baada ya kushuka kwenye basi la Simba sc nje ya kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija mjini Shinyanga-picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga



Wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na Msemaji wa Simba SC, Hajji Manara na kocha wa timu hiyoGoran Kopunovic na wametoa msaada wa maji na juisi na shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia kituo hicho ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo wao na timu ya Kagera Sugar kwenye ligi kuu Vodacom Tanzania bara utakaofanyika siku ya Jumamosi .

Wachezaji wa Simba SC wakiingia kwenye kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.
Simba SC inakuwa klabu ya kwanza nchini Tanzania kuwafikia watoto wenye ulemavu ambapo katika kituo hicho kuna watoto wenye ulemavu wa ngozi mpaka leo Ijumaa wapo 270.


Wachezaji wa Simba Sc wakipiga stori na watoto wenye ulemavu wa ngozi .

Wachezaji wakiwa wamebeba watoto wenye ulemavu wa ngozi

Kushoto ni Msemaji wa Simba SC, Hajji Manara akitafakari jambo 

Mchezaji wa Simba SC akionesha bango

Mkuu wa kituo cha Buhangija Jumuishi Peter Ajali akiwakaribisha wachezaji wa Simba sc ambapo alisema hiyo ni klabu ya kwanza  ya mpira nchini Tanzania kufika katika kituo hicho.

Eneo la tukio

Watoto wenye ulemavu wa ngozi wakiwa kituo

Kocha wa timu Simba sc Goran Kopunovic akizungumza jambo katika kituo hicho

Wachezaji wa Simba SC wakiwa wamebeba bango katika kituo cha Buhangija leo

Eneo la tukio

Wachezaji wa Simba sc wakiwa Buhangija

Mkuu wa kituo cha Buhangija Jumuishi Peter Ajali akiwa na mchezaji wa Simba sc wakiwa wameshikilia bango likisomeka “Imetosha mauaji ya Albino” ikiwa ni kauli mbiu ya timu juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanaoendelea nchini Tanzania.

Wachezaji wa Simba sc wakiwa Buhangija mjini Shinyanga

Mchezaji wa Simba SC Ibrahimu Twaha akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake ambapo alieleza kusikitishwa na vitendo vya mauaji ya albino na kujikuta akitoa machozi.

Kushoto ni Msemaji wa Simba SC, Hajji Manara akiwa amebeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi ambapo aliwataka watoto hao kutokata tamaa kwani wapo watu wenye ulemavu wa ngozi kama yeye wamefanikiwa katika maisha

Mchezaji wa Simba sc Emmanuel Okwi akipiga stori na watoto wenye ulemavu wa ngozi

Watoto wenye ulemavu wa ngozi wakiwa wamebeba bango

Zoezi la kugawa juisi likiendelea

Kocha wa timu Simba sc Goran Kopunovic katika pozi na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi leo

Wachezaji wa Simba sc wakiondoka kwenye kituo cha Buhangija-picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga