Thursday, April 2, 2015

CHRISTIAN BELLA KUFANYA USIKU WA MASAUTI

Mwanamuziki Christian Bella (katikati), akieleza jambo juu ya shoo yake inayotarajiwa kufanyika Aprili 18 mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Escape One, Mikocheni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni meneja wake John Mchaima ‘Simple’ na kulia ni mmoja wa waratibu wa shoo hiyo, Rehema Jones.
Mwanamuziki Christian Bella, akitoa kionjo cha wimbo wake kwenye kikao cha waandishi wa habari.
Meneja John Mchaima ‘Simple’, akielezea baadhi ya mikakati waliyojipangia katika kufanikisha shoo hiyo.
MWANAMUZIKI Christian Bella anatarajia kufanya shoo kubwa aliyoipa jina la Usiku wa Masauti, Aprili 18 Mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Escape One, uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Bella alisema katika usiku huo, pia atatambulisha video na audio ya wimbo wake mpya uitwao Nashindwa ambao tayari upo hewani.
“Natarajia kufanya shoo kubwa ambayo itanipa fursa ya kuwakutanisha wasanii wenzangu ambao wana nia safi ya kufanya mapinduzi kwenye muziki wetu wa dansi unaodaiwa kupotea, binafsi ninaumia sana ndiyo maana nimetumia kiasi cha dola 10,000 za Marekani kwa ajili ya kutengeneza video hii, naamini nitakuwa wa kwanza kwa kazi bora kama hii na ninaomba wenzangu waniunge mkono.”
Katika shoo hiyo, Bella amesema atasindikizwa na THT Band, Malaika Band pamoja na msanii kutoka nje ya  nchi aitwaye Alice ambaye tayari ameshathibitisha kuunguna naye kwenye shoo hiyo na itakuwa mara ya kwanza kwake kuja Tanzania na kufanya shoo kubwa.
“Naomba mashabiki waje kwa wingi ili waone ni jinsi gani ninavyopigana kuweka maboresho katika dansi, huku nikiamini kabisa muziki huu ni moja ya burudani inayopendwa  na watu wengi hapa Tanzania na ndiyo maana hata video ya wimbo wangu nimeifanya kimataifa zaidi ili kubadili ladha na mazoea ya muziki wetu,” alisema Bella.