Ni yale matukio ambayo huwa hayajitokezi sana, imetokea Indiana Marekani ambako Wanafunzi walikuwa kwenye tamasha la muziki wa Rock shuleni, wachache ndio walikuwa wanatumbuiza lakini muda mfupi baadae baada ya muziki kunoga wengine wakaja kucheza nao kwenye stage.
Kilichofata ni stage kuzama baada ya kutoboka na kufanya Wanafunzi zaidi ya 12 kujeruhiwa ambapo hii video hapa chini ni ya mtu aliyekuwa anarekodi tukio zima na inaonyesha live jinsi ilivyotokea mpaka ikazama na Wanafunzi hao.