Saturday, April 25, 2015

MSANII NAY WA MITEGO NA SHAMSA NI MKE NA MUME SASA!!,HEBU SHUHUDIA MWENYEWE

Musa Mateja
Mara baada ya kuelezwa kwamba wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wenyewe wakidanganya wana ‘projekti’, hatimaye majirani wamefichua kuwa mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’, sasa wanaishi kama mke na mume.
Mwigizaji Shamsa Ford na mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay’ wakizungumza jambo.
Baada ya kutonywa ‘mchapo’ huo, gazeti hili liliwadamkia nyumbani kwa Nay maeneo ya Kimara-Korogwe jijini Dar na kumkuta Shamsa akiwa na kanga moja.Mwanahabari wetu, baada ya kufika nyumbani hapo mishale ya asubuhi alikuwa bega kwa bega kuwafuatilia ambapo alifanikiwa kugundua kwamba wawili hao sasa wanaishi kama mume na mke.
Habari zilizopatikana zilidai kwamba, kwa sasa Shamsa hana muda mwingi wa kukaa nyumbani kwake kwani asilimia tisini kama si mia moja kabisa, anautumia kukaa na Nay nyumbani hapo.Mara kadhaa mwandishi wetu amekuwa akifika nyumbani hapo na kumkuta Shamsa akipika na kupakua huku akiwa na kanga moja huku wenyewe wakiitana mke na mume na kuoneshana mahaba motomoto.
.
..Wakipozi kimahaba.
“Kwani tatizo lipo wapi? Siwezi kufanya siri tena, sisi tupo kwenye uhusiano wa kimapenzi kama unavyotuona, nimeamua kumchagua Nay kwa kuwa anajua kupenda na kuthamini,” alisema Shamsa alipohojiwa na paparazi wetu.
Alipoulizwa Nay kulikoni ‘kumficha’ Shamsa nyumbani kwake, alifunguka:
“Yeah! Kwa sasa hakuna project tena, hapa ni mapenzi kwa kwenda mbele, sipendi kuwazungumzia wengine, napenda kuangalia uhusiano wangu upo vipi kwa sasa, ninampenda Shamsa.”
...Wakipata msosi.
Nay na Shamsa walianza uhusiano huo mara baada ya mwanamuziki huyo kudai kwamba alimnasa mpenzi wake, Siwema akiwa na mwanaume ndani ya sita kwa sita hivyo kuamua kuachana naye moja kwa moja na kujikuta akiangukia kwa mwigizaji huyo.