Hatimaye lile sekeseke la ndoa ya meneja wa wasanii wa Bongo Fleva wanaosimamiwa na Kampuni ya Endless Fame, Petit Man na mdogo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Esma Platnumz limemdondokea Wema Isaac Sepetu anayedaiwa kuitibua kiasi cha kuwatenganisha na kila mmoja kuchukua hamsini zake.
Habari kutoka chanzo chetu zilidai kwamba, Wema amehusika kwa asilimia kubwa kutibua ndoa hiyo kwani amekuwa akimtafutia mademu Petit Man, jambo ambalo Esma alilishtukia na kuamua kumbwatukia Wema kwa kuandika maneno makali kwenye mitandao ya kijamii.
“Kwa taarifa yenu Esma anamlalamikia Wema kuwa anamfanya mumewe kuwa mhuni kiasi kwamba anachukua mademu, tena marafiki zake na hata akimuuliza Petit Man anajifanya hao ni mashoga wa Wema.“Anapomkomalia, mara kadhaa umekuwa ukizuka ugomvi mkubwa na Petit Man anahama nyumbani kwake na kukimbilia kwa Wema,” kilisema chanzo chetu.Baada ya kunyetishiwa ‘infomesheni’ hizo, gazeti hili liliingia kazini kusaka ukweli wa mambo yanayodaiwa.
Lilianzia kwa Esma, alipopatikana alisema ni kweli hivi karibuni aliandika ujumbe kwenye Mtandao wa Instagram, ingawa kwenye maelezo yake hakumtaja mtu bali aliandika kwa hisia kama binadamu mwingine anavyoweza kuandika.
“Nani anasema nimemtukana mtu? Niliandika mambo ambayo nilijisikia mwenyewe lakini sikumtaja wala kumlenga mtu yeyote, kama kuna mtu alikwazika basi atakuwa anajichanganya mwenyewe.“Mimi sina tatizo na Wema na mambo ya familia yangu siwezi kumwambia kila mtu hivyo kama kuna ugomvi kati yangu na mume wangu hayo ni mambo ya familia yetu,” alisema Esma.
Kwa upande wake Wema alifunguka kwamba hajawahi kuongea jambo na Esma na kama kuna kitu aliandika kwenye ‘peji’ yake yeye hakuona.Alisema anachokumbuka ni kwamba aliongea naye (Esma) akiwa Hospitali ya Aga Khan Aghakan, Dar.
“Huwa siongei na Esma mara kwa mara kwani sina sababu sana ya kuwa naye kwa kuwa si mume wala bwana’ngu.
“Pia sijawahi kukwaruzana naye, sasa kama kuna kitu alisema, mimi namtafutia wanawake mumewe basi atakuwa anakosea kabisa,” alisema Wema.
“Pia sijawahi kukwaruzana naye, sasa kama kuna kitu alisema, mimi namtafutia wanawake mumewe basi atakuwa anakosea kabisa,” alisema Wema.