Friday, April 3, 2015

KUNA KILA SABABU DAVIDO ANANYIMWA SANA USINGIZI NA DIAMOND TAZAMA KISANGA ALICHOFANYA DAVIDO!!

BAADA YA SIKU CHACHE TU KUPITA KWA DAVIDO KUJIDAI HAMJUI KABISA DIAMOND ALIPOHOJIWA HUKO KENYA LEO HII KAJA NA KITUKO HIKI HEEE!!

Uhusiano kati ya Davido na Diamond Platnumz ulishavunjika siku nyingi kufuatia issue iliyotokea mwaka jana kwenye fainali za shindano la Big Brother Africa.
Davido na Diamond Platnumz akiwa studio mwishoni mwa mwaka juzi
Tukio hilo lilimfanya Davido aandike mfululizo wa tweets za mafumbo ambazo wengi waliamini kuwa ni madongo kwa Diamond aliyewahi kumshirikisha kwenye remix ya Number One iliyotokea kuwa hit namba moja Afrika miaka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kambi ya Diamond ilisisitiza kuwa hakuna ugomvi kati ya mastaa hao wawili na hata staa huyo wa ‘Nasema Nawe’ hivi karibuni aliwahi kuupa shavu wimbo mpya Davido kwenye Instagram.
Lakini vipi kama kweli Davido na Diamond bado ni washkaji? Kwa kile alichokipost Davido kwenye ukurasa wake wa Facebook, huenda wawili hao wakawa wanaendelea kupanga kufanya makubwa baadaye.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Davido amepost picha ya zamani akiwa na Diamond kwenye studio yake nchini Nigeria. Kwenye picha hiyo, Davido ameandika: I think I just recorded a sweeter love song than AYE .. Hmm this album yo.”


Picha hiyo imevutia comments nyingi japo asilimia kubwa ni za wakenya wanaomnyeshea mvua ya matusi! Yes, Wakenya hawataki kumsikia tena Davido!
HEBU PIA TAZAMA VIDEO ALIPOKUWA KENYA ALIULIZWA KUHUSU DIAMOND NA TAZAMA ALICHEJIBU DUUH!! ETI HAMJUI KABISA DIAMOND.

 

Hakuna shaka kuwa staa huyo wa Nigeria ana picha nyingi ambazo angeweka kuambatanisha na ujumbe huo. Hivyo, uchaguzi wa picha akiwa na Diamond unaweza ukawa na dhumuni maalum!