Friday, April 3, 2015

SASA LILE TIMBWILI LA MKALI NANI KATI YA DIAMOND NA ALI KIBA LAHAMIA KWA KINA DADA KUWAKILISHA KWA VIUNO DUUH!

Baada ya kuwa na sakata la muda sasa la mkali nani kati diamond na Ali kiba team hizi zimefikia hadi kwa kina dada sasa mara baada ya ali kiba kutoa wimbo wa chekecha na vimwana kuji cheketua kupitia video team diamond wakaona isiwe kesi na wao wakaporomosha mzigo wa nasema naye toka kwa diamond akiwa na Mwana mama Khadija kopa hapa napo kina dada wameanza kuwakilisha wimbo kwa kujirekodi wakimwaga mauno ya hatari tupu.

Hii haikutosha Mtu mzima diamond akakazia zaidi kwa kuonyesha kapania kweli kweli hilo shindano kwa kuandika kitu hichi kwenye kurasa yake ya instagram kudhihirisha yupo serious kweli kweli na viuno vya kina dada watao jirekodi video kucheza wimbo wake huu mpya wenye mahadhi ya pwani!!



Ndipo bila hiyana Team michepuko ikaona heri ikuletee ushudie mwenyewe kati ya hawa kina dada wa timu hizi mbili walio jirekodi video nani makaliii TEAM KIBA VS TEAM DIAMOND!!!