Mtoto mwenye umri wa miaka 13 amekamatwa usiku akiwa uchi kwa madai kuwa alikuwa akiwanga katika duka moja lililopo kijiji cha mpunguti Mkoa wa Mbeya.
Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mtoto huyo ni mzoefu kwa kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakipotelewa na fedha katika amzingira ya utata ambapo walitega mtego ili kubaini upotevu huo na kumbaini akiingia kwenye duka moja ambalo linadaiwa kuzindikwa.
Taarifa za awali kutoka kwa wakazi wa eneo hilo zilidai kuwa mtoto huyo alikuwa anaishi na bibi yake ambaye alimfukuza kutokana na tuhuma za ushirikiana na kukimbilia msituni kutokana na kukosa pa kuishi.
Inasemekana mototo huyo aliishi misituni kwa zaidi ya miezi mitano ndipo aliporejea na kuolewa lakini ndoa yake haikudumu kutokana na maisha kuwa magumu na akaamua kuanza mbinu za kichawi kwa kuibia watu.
Alianza kufungua kufuli za maduka kwa kutumia kidole gumba huku akiwa uchi na alinaswa na kupelekwa kwenye ofisi za kata ambapo anashikiliwa hadi sasa.