Kuna tukio limetokea katika Mkoa wa Lindi ambapo Mwalimu Mkuu wa shule moja ya msingi mkoani humo (Haikufahamika mara moja) ameamka asubuhi ya leo na kukuta jeneza limewekwa mbele ya mlango wa nyumba yake.
Wananchi wa eneo hilo nao wamepigwa na butwaa kwa tukio hilo. Taarifa zaidi zinasema Mwalimu huyo amedhamiria kuomba uhamisho wa haraka sana kutoka katika eneo hilo kwa sababu inaonekana wenyeji hawamtaki kutokana na yeye kushirikiana na serikali ya Kijiji kuwakamata wazazi wote ambao wanawaachisha shule watoto wao ili kuolewa.
Baadhi ya Waandishi waliopo mkoani humo wamesema wanafuatilia tukio hilo ingawa hadi sasa Polisi mkoani humo bado hawajathibitisha tukio hilo.