MTANGAZAJI mkongwe wa televisheni, Sauda Mwilima ambaye mumewe, Kauli Juma aliondoka mara tu baada ya kufunga naye ndoa kuelekea Afrika Kusini kikazi, amesema wa ubani wake huyo amesharejea na hivyo kuwakejeli waliokuwa wakisema kuwa ndoa yao ilikuwa ni magumashi.
Akipiga stori na paparazi wetu, Sauda alisema kwa sasa anaifurahia ndoa yake vilivyo baada ya mumewe kurudi Bongo baada ya kuwa Afrika Kusini kikazi kwa muda mrefu na baadhi ya watu kuzungumza mengi kuhusu ndoa yao.
“Nadhani watu sasa watajua kuwa siyo jambo zuri kuzungumzia kitu usichokijua, mume wangu amerudi na hakuna ninachokifurahia kama ndoa yangu. Ama kweli ndoa ni tamu,” alisema Sauda