Raia wa Tanzania wanaoishi Afrika Kusini sasa wanadaiwa kushika silaha tayari kwa mapambo dhidi ya vikundi vya raia wa Taifa hilo vinavyoshambulia wahamiaji wa Kiafrika.
Taarifa kutoka kwa Watanzania hao zimeeleza hatua hiyo imefikiwa baada ya kupatikana kwa taarifa zinazodai kuwa wenzao wawili wameuawa katika machafuko ya jiji la Durban ambayo chanzo chake ni mashambulizi yanayofanywa na raia wan chi hiyo dhidi ya wageni.
Mmoja wa Watanzania anayeishi Cape Town Pius Mbawala alieleza kuwa taarifa za mauaji ya wenzao zimewasikitisha sana na kwamba hadi sasa hakuna kiongozi yoyote wa ubalozi wa Tanzania aliyewasiliama nao ili kujua hali za usalama wao tofauti na balozi za nchi nyingine.
Mbalawa alisema kwa muda mrefu sasa maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini humo wamekuwa na uhusiano wenye shaka na Watanzania walioko huko tofauti na wanavyopaswa kujua ukazi wao kwenye Taifa hilo.
Alisema Raia wa Tanzania wanaoishi nchini humo wamejiunga katika makundi madogo madogo kulingana na maeneo wanayoishi kwa ajili ya kujilinda wenyewe na kila kundi hivi sasa limejihami kwa silaha.