Monday, April 20, 2015

WEMA, WOLPER WALEWA CHAKARI!,KISA MSONGO WA MAWAZO KIKO HAPA...ANGALIA WALIVYOKUWA JANA USIKU

Mastaa warembo kutoka Bongo Movies,  Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe, wamejikuta wakipiga ulabu hadi kulewa chakari, kisa kikielezwa kwamba wana msongo wa mawazo.
Wema, Wolper Walewa Chakari!,Kisa Msongo wa Mawazo
 
Gazeti la Risasi la jana, limeripoti kuwa tukio hilo lilijiri hivi karibuni, usiku mnene kwenye pati ya kuzaliwa (birthday) ya meneja wa kampuni ya Wema ya Endless Fame almaarufu Petit Man iliyofanyika kwenye nyumba ya jamaa mmoja maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao. Katika pati hiyo ambayo mbali na mastaa ilihudhuriwa na watoto wa mjini, watu waligonga msosi wa kufa mtu kisha vikafuata vinywaji.
 
Tofauti na ‘maraia’ wengine, Wema na Wolper walikuwa wakigonga vinywaji vikali hadi wakawa tilalila na kuanza kufanya vituko, jambo ambalo liliwashangaza wengi.Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivyo mastaa hao walivyozidi kucharuka tofauti na walipofika kwani walionekana wapole na wastaarabu kupita maelezo.
 
Baada ya ulabu kuwakolea walianza kupigana picha kwa simu kisha kukata mauno kabla ya Wolper kuzimika kufuatia kuzidiwa na ‘kinywaji’.Kwa upande wake Wema alimpiga vibao mwanaume shoga aliyetajwa kwa jina moja la Danny baada ya kutibuana kabla ya watu kuwaamulia.Ulipofika muda wa kuondoka mahali hapo, ilidaiwa kwamba Wolper ilibidi abebwe ili kupelekwa kwenye gari kwani alikuwa hajiwezi.
 
Uchunguzi wa gazeti hilo umebaini kwamba, mastaa hao wana msongo wa mawazo hivyo wanaona njia pekee ya kuwaondolea ‘stresi’ ni kunywa pombe.
 
Habari za ndani zilieleza kwamba, tangu Wema ameachana na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekuwa mtu mwenye mawazo na njia pekee ambayo huitumia ni kujipooza kwa pombe kali. “Ndiyo maana ana mpaka kaunta ya pombe kali nyumbani kwake,” alisema mmoja wa watu wake wa karibu (Team Wema).
 
Ilisemekana kwamba mbali na mawazo ya Diamond ambaye amehamia kwenye nyumba ambayo Wema alikuwa na mchango mkubwa wakati wa ujenzi, pia suala la jamaa huyo kutanua na mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ limekuwa likimpa wakati mgumu mwanadada huyo.
 
Habari zilieleza kuwa, jambo lingine linalompa Wema msongo wa mawazo ni suala la kukosa mtoto kila anapomtafuta akiamini kuwa watu wanajua yeye ni mgumba.Pia ilielezwa kwamba kuna suala la kuishiwa na kuogopa kufilisika kwani kwa sasa filamu hazilipi na bado anataka kuendelea kuwa na heshima ya kuitwa Madam hivyo njia pekee anayoona inafaa kutuliza mawazo ni kunywa pombe.
 
Kwa upande wake Wolper uchunguzi ulionesha kwamba, kwanza anapenda fedha hivyo kukosa tenda za kuigiza na kuanguka kwa soko la filamu za Kibongo kumemsababishia msongo wa mawazo kama ilivyo kwa Wema kwani naye anataka kuishi maisha ya kistaa ambayo hayawezekani bila kuwa na mshiko.

Akizungumzia hali hiyo, Wolper alikiri kuwa na mawazo mengi huku akihisi kuwa huenda amelogwa