Staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel ambaye hivi sasa ni mjamzito ameeleza kuwa kila saa na kila siku anamuomba Mungu amjaalie ajifungue salama maana maneno ya watu yamekuwa yakimtisha.
Akizungumza na gazeti la Ijumaa hivi karibuni nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar, Aunt alisema kuna watu ambao wamekuwa wakimuombea mabaya kutokana na chuki zao lakini yeye anaamini Mungu ndiye kila kitu kwake.
“Wapo watu ambao wanaisengenya mimba yangu, wananisema vibaya, wananiombea mabaya kiasi cha kunipa hofu. Lakini yote kwa yote namuomba Mungu nijifungue salama,” alisema Aunt