Sunday, May 17, 2015

BLACKETT AITIBULIA MAN UNITED DAKIKA ZA LALA SALAMA, AWAFUNGIA ARSENAL WAPATA SARE OLD TRAFFORD

TIMU ya Manchester United imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Old Trafford.
United walikaribia kushinda mechi hiyo kama si Tyler Blackett kujifunga katika harakati za kuokoa krosi ya Theo Walcott na kuisawazishia The Gunners dakika ya 80.
United ilitangulia kupata bao kupitia kwa Ander Herrera dakika ya 30 akimalizia krosi ya Ashley Young.
Kipa Victor Valdes aliidakia kwa mara ya kwanza Manchester United akitokea benchi kuchukua nafasi ya David de Gea aliyeumia. Kwa matokeo hayo, Arsenal inaendelea kuizidi pointi mbili Manchester United katika nafasi ya tatu.
Kikosi cha Manchester Utd kilikuwa; De Gea/Valdes dk74, Valencia, Smalling, Jones, Rojo/Blackett dk73, Blind, Mata, Herrera, Fellaini, Young na Falcao/van Persie dk60.
Arsenal; Ospina, Bellerin/Walcott dk72, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla/Wilshere dk72, Ramsey, Ozil, Sanchez/Flamini dk90 na Giroud.
Marcos Rojo rises above Olivier Giroud to win a header as the hosts made a strong start in the race to avoid a Champions League qualifier
Marcos Rojo wa Man United akienda hewani zaidi ya Olivier Giroud wa Arsenal kupiga mpira kichwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo