Monday, May 25, 2015

Diamond amesharekodi collabo na msanii mkubwa wa Marekani, hutaamini ni yupi!

Muimbaji huyo alikuwa akiongea
kwenye kipindi cha 360 cha Clouds TV
leo asubuhi ambapo aliulizwa ni
msanii gani wa nje ya Afrika
anayependa kufanya naye kazi.
Diamond alidai kuwa tayari msanii
anayemkubali zaidi nchini Marekani
ameshafanya naye kazi japo
hakupenda kumtaja tena.
Aliombwa amtaje msanii mwingine
tofauti na huyo na kusema wasanii
watano anaowapenda zaidi nchini
Marekani ni Nicki Minaj, Chris Brown
na Usher Raymond na kwamba
mmoja kati ya hao tayari ameshafanya
naye ngoma!
So ubashiri wetu ni Nikki Minaj!