MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini, Frola Mbasha ameijunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers mjini Dar es Salaam jana, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alisema kuijunga kwa Mbasha katika chama hicho kutasaidia kuhamasisha wasanii wengine ambao wamekuwa wakitumiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM), bila kupata mafanikio.
” Idadi kubwa ya wasanii nchini, wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM bila kupata mafanikio ya aina yoyote…Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee.
Naye Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alisema siku Serikali itakapowasilisha muswada wa Sheria wa Vyombo vya Habari bungeni, wabunge wa chama hicho na wale wanauounda Umoja wa Katiba ya Wananchi ( Ukawa) watafanya vurugu ili kuhakikisha haupiti.
Alisema baadhi ya vipengele vya muswada huo vinakandamiza waandishi na wananchi kupata habari.
” Siku Serikali ikiwasilisha Muswada wa Vyombo vya Habari,mimi na wabunge wangu tutafanya vurugu hadi unaondolewa bungeni,” alisema Mbowe
Naye Naibu Katibu Mkuu- Bara, John Mnyika alisema Jiji la Dar es Salaam lina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko licha ya kuwepo kwa wizi mkubwa kura wakati wa uchaguzi.
” Idadi kubwa ya wasanii nchini wanateseka bila ya kujijua, hii inatokana na kutumiwa na CCM Vila ya kupata mafanikio ya aina yoyote, hivyo basi Frola inabidi uwaelimishe ili waweze kujiunga na chama chetu,”alisema Mdee.