Tuesday, May 26, 2015

Kajala kaweka picha ya Wema na Petit Man kwenye ukurasa wake @Instagram, na hiki ndicho alichokiandika !

NEWKAJALA
Staa wa Bongo Movie Kajala Masanja aliwahi kuwa mgeni wangu kwenye studio za #TZA na millardayo.com katikati ya mwezi April 2015, nakumbuka jibu lake kuhusu ishu ya Wema kutokua na uwezo wa kuzaa; “Mwandishi alinipiga mwandishi akaniulizaa kuhusu hiyo kitu.. nikamwambia namwonea huruma, yeye bado mdogo asikate tamaa kwamba hatozaa.. labda atafute Doctor mzuri kama kweli ana nia ya kupata mtoto atapata..
Saa moja muda mfupi uliopita kaandika post yenye ujumbe huu alafu kaweza na picha yaWema Sepetu na Petit Man>>> “BINADAMU TULIUMBWA KUISHI KATIKA MISINGI YA UBINADAMU NA SIO UNYAMA KAMA WAISHIVYO WANYAMA WA PORINI LEO NAOMBA KUSEMA KUTOKA MOYONI MWANGU.. NAJUA KABISA NINA WAZAZI WANGU NDUGU ZANGU NA ZAIDI SANA MUNGU WANGU ILA KUNA WATU MPAKA NAKUFA KAMWE SINTOWASAHAU KATIKA KUTA ZA MOYO WANGU KATIKA KIPINDI CHANGU KIGUMU NILICHOPITIA MLIKUWA NEMBO NA MBONI KUBWA KATIKA KUOKOA MAISHA YANGU… NAPENDA KUSEMA KUWA HATA KWA HAYA YOTE TUNAYOPITIA BADO NI MADOGO SANA KUFICHA THAMANI YENU MLIYOIJENGA JUU YANGU..NAKUMBUKA SANA MLIPOJITOA KWA AJILI YANGU MLIPOJINYIMA KWA AJILI YANGU MLIPOPIGANA KWA AJILI YANGU,MLIVYOFEDHEHEKA KWA AJILI YANGU YOTE HAYO NAYAKUMBUKA NA NAMSHUKURU MUNGU KWANI NAONA KABISA MLILETWA DUNIANI KWA SABABU NYINGI NA MOJA YA SABABU ILIKUWA KUNIOKOA KATIKA KIPINDI KIGUMU KATIKA MAISHA YANGU.LEO HII TAREHE 25.5.2015 NAPENDA KUSEMA KWA UMMA NA ZAIDI KWA MUNGU WANGU KUWA NAWATHAMINI NAWAPENDA NA NASHUKURUUU SANA KWA YOTE MLIYOFANYA JUU YANGU.. NAWAOMBEA KWA MUNGU MUENDELEE NA MOYO HUO HUO KWANI NAAMINI KUNA WENGI BADO WANAWATEGEMEA ILI KUKOMBOA MAISHA YAO KWA WAKATI ALIYOPANGA MUNGU HATA KITABU CHA DINI KILISEMA KUWA “huwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona” NAJUA SIKU MOJA TUTAISHI KAMA ZAMANI.. AHSANTENI” >>> @