Staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja ameweka wazi kuwa mipango yake ya kuzaa watoto iko palepale na kwamba safari hii angependelea kuzaa watoto mapacha.
licha ya kwamba Kajala ana binti yake aitwae Paula,atahakikisha anamtafutia wadogo zake kwani hata yeye amekaa kweny falimia ya watoto wengi na angependelea na yeye kuwa na familia kubwa.Kajala amebainisha kwamba hafikirii kupata mtoto na mme wake ambae kwa sasa yuko gerezani bali anatafuta mwanaume mwenye malengo ya maisha na mwenye kujali familia.
Licha ya kuwa na mipango yote hiyo Kajala ameelezea ugumu anaoupata katika lengo lake la kuilea hiyo familia kwani hadi sasa binti yake paula anakosa raha kutokana na skendo zinazotengenezwa dhidi yake.Amesema hali hyo iimekua inamnyima raha binti yake huyo hata anapokua shuleni kwani wenzake humnyooshea vidole kila wakati kutokana na taarifa ambazo alisema si sahihi kuhusu mama yake..
Mwananchi