Saturday, May 23, 2015

HALI NI TETE UDOM, KWAGEUKA KAMA VITANI



Licha ya jitihada zilizofanywa na Naibu Waziri wa Afya na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuwatuliza wanafunzi wa kitivo cha elimu wasigome na kwamba Serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha wanapata fedha hizo kwa haraka, jitihada hizo hazijazaa matunda kwani wanafunzi walisisitiza wataendelea na mgomo wao mpaka pale watakapolipwa fedha zao sababu hawawezi kusoma wakiwa na njaa na imekuwa kawaida ya serikali kuwadanganya.
Leo hali imekuwa ni tete zaidi baada ya mgomo wa
kususia masomo Chuo Kikuu cha Dodoma kuendelea kushika kasi. Majira ya saa nne asubuhi hali imeendelea kuwa mbaya zaidi huku wanafunzi wakihitaji kuelekea utawala Mkuu wa Chuo ili kuitiwa Waziri Mkuu wa Nchi, Mh; Pinda.

Baada ya muda mfupi hali ilichafuka na askari wwakaanza kushambulia kwa kuwatawanya wanafunzi, huku wakiwataka warudi mabwenini kwao.

Polisi walifanikiwa kuzima maandamano kwa kutumia maji ya kuwasha pamoja na mabomu ya kutoa machozi,ambapo taarifa za awali zinaeleza kwamba  wanafunzi wengi wameumia na wengine wamekamatwa.