Mwaka juzi kulikuwa na sintofahamu kuhusu nani achinje iliyosababisha kifo cha mchungaji moja kanda ya ziwa. Wakati sarakasi hiyo ikiwachanganya watanzania, katibu wa Bunge Thomas Kashillah aliibuka na kusema Bunge halitaoneshwa tena kwenye Runinga. Mjadala ukahama kutoka uchinjaji na kuwa Bunge kutooneshwa. Serikali ikafanikiwa, kombe likafunikwa na mwanaharamu akapita.
Mwaka 2013 mvua kubwa kuliko hii ya mwaka huu ilinyesha na kusababisha mamia ya watu kulala njiani na njaa wakiwa na watoto. Njia zote za kuingia Dsm zilifungwa na maji na matokeo yake watu wakawa na hasira na serikali kutosimamia miundo mbinu vizuri jambo lililosababishia wao kupata madhara yale. wakati hayo yakipamba kwenye vyombo vya habari ghafla tukaambiwa Makamu wa Rais, waziri magufuli na mkuu wa mkoa wa Dsm wameanguka na helikopta. kama kwaida Mjadala ukahama kwa walioanguka na helikopta. Mwanaharamu akapita tena. Ikumbukwe kuwa hakuna kati ya walioanguka na helikopta aliyenda hospitali wala picha ya helikopta iliyoanguka haikuonekana mpaka leo kama kaburi la Daudi Balali wa EPA iliyoibuliwa na Dr Dlaa.
Wakati wa Bunge la katiba, Tundu Lissu na UKAWA waliibua madudu mengi kuhusu muungano hasa pale walipohoji lilipo kaburi la waasisi wa muungano amabao ni Hanga na wenzake. Wakati mjadala huo ukishika kasi Dodoma, ghafla serikali ikaibuka na ugonjwa wa Dengue. Tukaambiwa wamekufa watu wawili mara watatu wakati malaria inaua zaidi ya watu watatu kila siku achilia mbali hao watatu hata kama ni zaidi ya watatu waliokufa mara moja na Dengue. Baada ya hoja ya Muungano kupita Dengue nayo ikayeyuka bila maelezo ya kutosha.
Je, watu wameshajiuliza kwanini magaidi feki wa amaboni walikuja wakati hoja ya ESCROW ikivuma? Tuliambiwa kuna askari wetu wamekufa. Je, akina nani kwa majina na walizikwa wapi na lini? Nani ameona picha hata moja ya askari wetu?
Mifano ya usanii huu wa serikali kuibua hoja ili kujilinda au kufunika udhaifu wake ni mingi sana.
Huko nyuma nilishaandika zaidi ya mifano kumi ya namna hii. Mifano hii michache inatosha kujenga hoja yangu. Kwa nini nimeyaeleza yote hayo??
Jana jioni nilimsikia kwenye ITV mwenyekiti wa MOAT ndugu Reginald Mengi akilalamikia serikali kutaka kupeleka mswada wa uhuru wa habari ambao moja ya kipengele chake kinavilazimisha vyombo vyote vya habari vikiwepo ITV, STAR TV, Chanel ten nk vijiunge na TBC saa mbili usiku kwa taarifa ya habari. kwamba vyombo vingine (TV zingine) havipaswi kuwa na taarifa yao ya habari wenyewe badala yake sheria itawalazimisha wajiunge na TBC. Je, hili linawezekana??
Mimi kama MIKAEL AWEDA sidanganyiki na hili. Nina wasi wasi nalo. Siamini kabisa nikirejea mifano tajwa hapo juu. Kwa maoni yangu taarifa hii imeletwa ili kubadilisha au kusahaulisha au kufunika mjadala wa ufisadi wa zaidi ya trilioni moja ulioibuliwa na Chadema baada ya kuchambua ripoti ya CAG. Kwa hiyo, taarifa hii imeletwa makusudi wakati bunge na vyombo vya habari vikijadili ufisadi huu wa serikali. Nijuavyo, Bungeni wakishamaliza taarifa hii ya TV zote kujiunga na TBC saa mbili jioni nayo itayeyeka kama taarifa ya Dengue, hoja ya kashilillah ya Bunge kutooneshwa na TV au helikopta kuanguka bila majeruhi wala picha yake kuonekana.
Nihitimiasha kwa kusema kuwa ninahitaji muda zaidi kuamini hili vinginevyo mwana wa Aweda hadanganywi na janja ya kufunika wizi wa matrilioni yaliyoibwa na viongozi wa serikali kwa kuibua hoja mbadala.
Nawasilisha
Mikael Aweda
0784 583 330
22/05/2015