Saturday, January 3, 2015
BAADA YA NIKKI MBISHI KUTANGAZA KUACHA MUZIKI, HAYA NDIO MANENO YA CHID BENZ
Baada ya msanii wa Hip Hop Nikki Mbishi aka Baba Malcom kutangaza kuwa ameacha kufanya kazi ya muziki sasa Chid Benz amekanusha taarifa hizo na kusema kuwa ameshafanya mazungumzo na msanii huyo na kumtaka asichukue uamuzi huo mapema kwani hata yeye amepitia katika changamoto hizo.
Chid Benz alichukua nafasi hiyo kuwataarifu mashabiki wa muziki kupitia ukurasa wa facebook na kuandika
‘Nakanusha habari za Nikki mbishi kuacha mziki,nimeongea nae kama kaka na kumgusia mengi,najua amenielewa na nimemwambia asikubali wale wanaomkubali waanze kukubali wengine.mimi nimekumbana na vingi na watu weengi waliaminishwa kama nimeshushwa kimziki,jimefanyiwa mengi ambayo kwa muda ule nsingeweza kuelezea kila mtu nini kinaendelea,so if kikitokea kibaya kinatangazwa mpk kwenye taarifa za habari mbona mziki hauchezwi?ningekua sina nguvu hio nisingesumbua watu kuniweka front page..but bado nipo na nimekomaa.na naishi na naona wanaopewa kipaumbele na najua bado mimi ni mimi.Iron'
~Udaku Special