Friday, May 22, 2015

MIUNDOMBINU MIBOVU YASABABISHA AJALI DAR

Muonekano wa sehemu ya barabara ilivyomeguka.
Daladala iliyokwanguliwa wakati wa ajali hiyo.
Trafiki akikagua eneo la tukio baada ya daladala hizo kugongana.
Taswira kamili ya eneo hilo lililoharibiwa na mvua.
KUFUATIA mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha barabara kumegeka katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar, hali hiyo imesababisha ajali ya daladala maeneo ya Tabata-Chama.
Ajali hiyo ilihusisha daladala aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T 401 AHC iliyokuwa ikitokea Mnazi Mmoja kuelekea Tabata na Coaster yenye namba za usajili T 129 CVP iliyokuwa ikitokea Tabata kuelekea Mnazi Mmoja ambapo kutokana na barabara hiyo kumeguka, walilazimika kutumia nyia moja hivyo kujikuta wakigongana.
Kwenye ajali hiyo, hakuna mtu aliyeumia lakini abiria waliokuwemo kwenye daladala hizo, waliishauri serikali iongeze juhudi haraka kurekebisha miundombinu iliyoharibiwa na mvua zilizoisha hivi karibuni.