
Muimbaji wa ‘Ole Themba’ Linah Sanga amewafungukia followers wake wa
Instagram baada ya kuchoshwa na masimango ambayo amedai yamemtoa
machozi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye followers 254,256 Linah ameandika ujumbe huu mrefu:
“Jamanii nimechoka Na kufuru zenu, hivi naomba niulize ufupi wangu,
kukomaa kwangu, mkorogo wangu vinawahusu nini? Ni naomba mfatilie kazi
zangu tu vingi be ni vitu vya kawaida kila binadamu kuambiwa kasoro
zake! Hvi wale ambao Hawana mikono Na miguu Na wao walie vipi kwa Mungu?
Namshukuru hivi nilivyo. Mbona mnapenda kutoa hukumu kama nyie ndyo
Israeli?! Ifike kipindi tukumbuke kila mtu anamaisha yake! Naona
mnaandamana sana Na maisha yangu. Kuna ambae hata alimsaidia mama yangu
wakati anapush hospitali? Hivi kumbukeni mnawazazi pia Na nyinyi
mlizaliwa pia,kama nyie Mungu basi nibadilisheni mniumbe mtakavyo, nyie
ni kina baba Na kina mama wa badae kumbukeni mtazaa Na nyinyi then
tuone! Chozi langu hili haliendi bure!! U will pay it back maana
nimechoka Na masimango yenu. “