Na Brighton Masalu
SIKU chache baada ya kuripotiwa kutengana na mkewe, msanii wa filamu za Bongo, Jimmy Mafufu ameibuka na ‘kuachia silabi’ zinazoashiria kumpa masharti magumu mwandani wake huyo.
SIKU chache baada ya kuripotiwa kutengana na mkewe, msanii wa filamu za Bongo, Jimmy Mafufu ameibuka na ‘kuachia silabi’ zinazoashiria kumpa masharti magumu mwandani wake huyo.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu juzi, Mafufu alisema kwa kuwa mkewe aliamua kuita waandishi wa habari wakati wa kuondoka hata wakati wa kurejea inabidi awaite laa sivyo abaki huko huko kwao.
“Kama alivyoondoka kwa mbwembwe nyingi na kuita waandishi wa habari, hata akitaka kurudi awaite pamoja na ndugu zake wamsindikize, tofauti na hivyo siwezi kumpokea wala sifikirii kurudiana naye,” alisema Mafufu.