Wednesday, May 27, 2015

PAMOJA NA UJANJA WOTE HUO LKN TUNDA MAN ALIZWA NA VIBAKA KIZEMBE ZEMBE


Nyota wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’.
VIBAKA ambao hawakufahamika mara moja mwishoni mwa wiki iliyopita, walivunja kioo kidogo cha gari la nyota wa Bongo Fleva, 
Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ na kumkomba vitu mbalimbali vikiwemo power window, kompyuta mpakato na fedha katika tukio lililotokea Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Katika usiku ambao msanii huyo ilikuwa apande na kufanya shoo katika klabu ya Kakala, wezi hao walivunja kioo cha gari yake aina ya  Verossa yenye namba T 420 CEP na kufanya uhalifu huo, kitendo kilichosababisha ashindwe kufanya onyesho hilo.
“Nimelizwa, roho inauma sana wamechukua na pesa shilingi 35,000 ambazo zilikuwa juu ya dashbod, wamebakisha elfu tisa tu” alilalamika Tunda Man ambaye alisema tukio hilo liliripotiwa katika kituo cha Polisi Kigamboni.