Thursday, May 28, 2015

Serekali Yatoa Kauli Yake Juu ya Uvaaji Mbaya wa Shilole..Yasema Atachukuliwa Hatua Baada ya Kujieleza

Serikali imeahidi kumchukulia Shilole kufuatia kusambaa kwa picha zake chafu zilizopigwa wakati akitumbuiza nchini Ubelgiji.

Akizungumza bungeni Dodoma leo, Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia, wakati akijibu hoja za wabunge baada ya kusoma makadirio na matumizi wa wizara hiyo, alisema tayari serikali imeliagiza baraza la sanaa taifa BASATA kufanya naye mahojiano.

Tumemtaka ajieleze kupitia BASATA, akishajieleza serikali itachukua hatua na niombe mheshimiwa spika kupitia bunge lako tufuku, kuliomba radhi kwa upande wa serikali kwa kitendo kilichofanywa na mwanamuziki yule. Sio maadili yetu na nimesema akishajieleza serikali itachukua hatua yake,” alisema Juma Mkamia.