Kioja hicho kilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa New Maisha Club, Oysterbay jijini Dar kulikokuwa na shoo ya Mrs. Mabeste Charity iliyohudhuriwa na mastaa mbalimbali wa filamu na muziki.
Katika hali ya kushangaza zaidi, Mwarabu huyo alipanda jukwaani hapo na kumtuza kabla ya kumkumbatia na kumganda kwa muda mrefu kama ruba huku akionekana kumnong’oneza hali iliyozua miguno na maswali mengi.