Thursday, May 14, 2015

Mgahawa Wauza Nyama ya Binaadamu Nigeria..Wamiliki Wakamatwa

Mgahawa mmoja nchini Nigeria katika jimbo la
Anambra umefungwa kufuatia viongozi wenye
mamlaka nchini humo kung’amua kwamba
moja ya vyakula vinavyouzwa mgahawani
humo ni nyama ya binaadamu.
Polisi walipoitwa mgahawani hapo waliona
vichwa viwili vya binaadamu vipya vyenye
kuchuruza damu wakati walipokuwa
wakiwakamata watu kumi na mmoja kutoka
mgahawani hapo akiwemo mmiliki wa
mgahawa huo,pia walikamatwa wanawake sita
na wanaume wane, baada ya wasamaria wema
kutoa taarifa hizo za kustaajabisha!
Damu zilizokuwa zikivuja kwenye vichwa hivyo
vya wanaadamu,vilikuwa vimefungwa kwenye
mifuko ya Rambo.
Polisi pia wamekamata bunduki aina ya AK-47
na silaha nyinginezo,seti ya magurunedi na
simu kadhaa za kila aina wakati walipokuwa
wakiwakamata watu hao.
Kila wakati nilipokuwa nikienda sokoni,na
sababu kubwa hasa hoteli hiyo iko karibu na
sokoni,nimekuwa nikishuhudia harakati za
ajabu za watu kuingia na kutoka hotelini
humo,watu wachafu na uchafu wao mwilini ni
ule usioeleweka,hivyo sikushangazwa polisi
walipogundua biashara hiyo haramu mapema
wiki hii, anasema mkaazi wa eneo hilo.
Mchungaji mmoja akiwa katika mshtuko
mkubwa baada ya kugundua kuwa alikuwa
amekula nyama ya binaadamu,aliamua kwenda
polisi kupeleka malalamiko yake .
Aliwaambia kuwa alikwenda kwenye mgahawa
wa hoteli hiyo asubuhi na mapema,baada ya
kupata staftahi,akaambiwa kwamba pande la
nyama alilokula gharama yake ni naira 700
sawa na paundi mbili unusu alistaajabu
mno.sikufahamu kuwa nimeuziwa nyama ya
binaadamu nikaila na kwamba ilikuwa ghali
sana.
Taarifa za watu nchini Nigeria kula nyama za
watu zimekuwa ni uvumi wa muda mreefu,
lakini hii ni mara ya kwanza mgahawa kuamua
kuuza nyama za binaadamu tu.